Wednesday, February 15, 2012

............UKURASA MPYA WAJA.......

MWANDISHI wa miswada ya filamu wa kutumainiwa Swahiliwood, Ali Yakuti, amesema filamu ya Respect of Nyerere inafungua ukurasa mpya kwa filamu za Tanzania na inaweza kuwa chachu kwa wasanii na watayarishaji wengine kutengeneza filamu kwa ajili ya viongozi wetu.

Nimefurahi sana kwa wazo la kijana Steve Nyerere kwa kuwa ni mmoja kati ya watayarishaji wenye mtazamo wa mbele hasa kwa kukubali kutengeneza filamu zao kwa kutumia viongozi wetu ambao wamelijenga Taifa na kuweka historia na wamekuwa moja kati vielelezo katika Taifa hili. Filamu ya Respect of Nyerere inadhihirisha hili, anasema Ali.

Filamu hiyo pamoja na kufanikiwa katika kuenzi na kudumisha viongozi, pia utayarishaji wake umezingatia mambo muhimu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha sehemu muhimu zinatumika ikiwa ni pamoja na kufika Butima katika nyumba ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili kuirekodi.

Walioshiriki katika filamu ya Respect of Nyerere ni Halima Yahaya Davina, Ruth Suka Mainda, Hashimu Kambi Ramsey, Steve Nyerere, na wasanii wengine kibao.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms