Thursday, February 23, 2012

..........SOMALIA BADO KWA MOTO......

Majeshi ya Ethiopia na yale ya serikali ya mpito ya Somalia yameuteka mji wa Baidoa ambao ni mojawapo ya ngome kuu ya wapiganaji wa Al Shabaab ambapo Walioshuhudia wamesema magari 50 vikiwemo vifaru vya kivita viliingia mjini Baidoa bila upinzani wowote.
Kundi la Al-Shabaab ambalo lilijiunga rasmi ya mtandao wa al-Qaeda limethibitisha kuwaondoa wapiganaji wake kutoka mji huo ambapo pia Wapiganaji hao wameonya kuanzisha mashambulio ya kujitoa mhanga dhidi ya majeshi ya kigeni.
Kutekwa kwa mji wa Baidoa ni pigo kubwa kwa Al Shabaab kwani ni makao ya mmoja wa viongozi wa kundi hilo Abu Mansoor na baadhi ya wanachama wengine wa juu.
Wakati huo huo Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, linatarajiwa kupiga kura ya kuidhinisha jeshi la kulinda usalama nchini Somallia kuongezwa kwa zaidi ya wanajeshi elfu tano.
Hii itafikisha idadi ya wanajeshi wote wa kulinda amani walio Somalia kufikia 17,731. Kwa wakati huu kuna wanajeshi elfu kumi na mbili wa kigeni nchini humo ambapo Kura hiyo ya Baraza la Usalama kutaipa fursa jeshi la Kenya ambalo kwa sasa liko nchini Somalia likipambana na Al shabaab ,nafasi ya kupigana chini ya mwamvuli wa jeshi la Umoja wa Afrika.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms