Wednesday, February 15, 2012

............SHILOLE AWA MKATA VIUNO........

MWIGIZAJI wa kike katika tasnia ya filamu Swahiliwood Zuwena Mohamed Shilole amesema kuwa baada ya kufanya vizuri katika filamu na kuonyesha upinzani kwa waigizaji wengine wa kike na kuwafunika, ameingia katika fani nyingine ya muziki.

Kila mtu anamjua Shilole katika tasnia ya filamu kwa uwezo wake wa kuigiza, naweza kusema sina mpinzani katika filamu, nafasi yangu ipo kubwa, lakini katika kuonyesha uwezo wangu kwa sasa nipo katika maandalizi makubwa ya kurekodi albamu ya muziki na nyimbo mbili zipo tayari na zinafanya vema redioni, anasema Shilole.

Msanii huyo anasema kuwa anatarajia kuandaa albamu yenye nyimbo sita, na kwamba katika nyimbo zilizobaki anatarajia kuwashirikisha wasanii kama Dully Sykes na Diamond ili kuikamilisha albamu yake ambayo baadaye ataifanyia filamu.

Nyimbo alizotoa ni Mwanaume dada aliomshirikisha AT, na 'Nyumba za Kupanga' aliomshirikisha Q Chillah.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms