Friday, February 10, 2012

..........SANDHU AMUUNGA MKONO SINTAH........ SANDHU
SINTAH

NYOTA kutoka Maisha Plus, Steven Sandhu ametamka kitu ambacho wasanii wa filamu za Bongo wakikisikia wataguna na kurusha mikono kupuuza.

Sandhu amewaasa wasanii wa filamu kujiendeleza kielimu ili kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo.

Wasanii wengi tunahitaji kujiendeleza zaidi kutokana na hali ya utandawazi, kabla sijaingia katika uigizaji nilijua kuwa wasanii wengi wana taaluma katika fani hiyo, lakini wengi wao wanatumia sana vipaji kuliko taaluma.

Nahisi hali hiyo inaweza kuwa ni tatizo kwa sababu msanii akikutana na msanii wa kimataifa wanaweza kushindwa kufanya kitu kwa pamoja, anasema Standhu.

Msanii huyo amekuwa kivutio katika filamu nyingi kutokana na staili yake ya nywele.

Anasema aliingia katika uigizaji bila kupewa mbinu za uigizaji na alikuwa anajiona kama yupo sawa.

Hata hivyo, anasema alipokutana na muongozaji wa filamu, Karabani na kufundishwa wakati akiigiza filamu ya CPU, alijiona kumbe bado katika uigizaji.

Naamini kuwa hali hii ndiyo ipo kwa wasanii wengi nchini, anasema.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms