Monday, February 20, 2012

.........ODAMA AKARABATI MWILI WAKE......

MWANADADA anayefanya vizuri ndani ya bongo movie, Jannifer Kyaka ‘Odama’, amesema kuwa anajitahidi kuukarabati mwili wake ili awe mrembo zaidi kwa ajili ya maandalizi ya filamu yake mpya ambayo bado hajaipa jina.

Kupitia mmoja wa waandishi wa blog hii akutana na mrembo huyo, kwa ajili ya kuzungumza mambo juu ya urembo wake, ambapo alisema kuwa anafanya utaratibu wa kuongeza zaidi mvuto ndani ya mwili ili aweze kucheza filamu ambayo itaelezea zaidi muonekano wa msichana.

Odama alisema wapo baadhi ya watu ambao watasema juu ya mabandiliko yake lakini kwa upande wake hashindwi kufanya mambo kwa kuongopa watu ambao hawamsaidi kitu chochote ndani ya maisha yake.

“Nipo katika maandalizi ya filamu zangu kadhaa lakini kazi hizi zitanihitaji nicheza kama mwanamke mrembo zaidi hivyo sasa nipo katika maandalizi ya kununua dawa ambazo zitanifanya nionekane mrembo zaidi ya hivi nilivyo sasa,” alisema.

Hata hivyo Odama, alienda mbali na kudai kuwa baada ya kucheza filamu hizo anaweza kuwa mtu maarufu Duniani kote kwa sababu kazi hizo zinaweza kuuzwa Dunia nzima.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms