Sunday, February 12, 2012

........MWIMBAJI HOUSTON AFARIKI DUNIA........JAMANI HUU UDONGO UMEMEZA WATU.......

  Houston akiwa kwenye picha ya pamoja na mmewe na mtoto wao
Hii ndo hoteli alipokutwa na mauti mwimbaji Houston 
 
Mwimbaji Whitney Houston amekutwa na mlinzi wake akiwa amefariki dunia bafuni kwenye hoteli The Beverly Hilton.
Hakukua na dalili zozote za uhalifu, yani hakukua na dalili zozote kama ameuwawa au hilo tukio limefanywa na mtu yoyote japo polisi walikuta chupa ya vidonge vya dawa za hospitali.
Kwa sababu mwili wake ulikutwa nje ya bathtub itabidi polisi wachunguze kama kifo chake kimesababishwa na kuzama kwenye maji ya bathtab au alioverdose dawa.
Mama mzazi wa Whitney amesema alizungumza na mtoto wake dakika 20 mpaka 30 kabla hajafariki dunia, na hakukua na tofauti yoyote kwenye mazungumzo ya Whitney, alikua anaongea kawaida.
Whitney alizungumzia kuhudhuria Clive Davis’ pre-Grammy party na alizungumza na binamu yake Dionne Warwick saa chache kabla kwamba wasiachane, wahakikishe wanakaa meza moja kwenye party.
Mwili wa Whitney houston aliekua mtumiaji mkubwa wa dawa za kulevya, ulikaa kwenye gorofa ya nne mpaka saa tano usiku toka alipofariki saa nne usiku, ambapo katika hiyo hiyo floor ya nne ndio kulikua kuna hiyo party ambapo Mwili wake ulichukuliwa na wakati Party hiyo ikiwa inaendelea.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms