Saturday, February 4, 2012

........MSAFIRI DIOUF KUREJEA KWENYE AFYA YAKE........

RAPA mahiri wa bendi maarufu Bongo ya Twanga Pepeta, Msafiri Hassan 'Diouf' ameanza kutumia dawa za miti shamba ili kuboresha afya yake ambayo ilidorora katika miezi ya karibuni.

Mwanamuziki huyo amekuwa akituhumiwa kwa kunywa vinywaji vikali ambavyo vimemdhoofisha na kushindwa kuwa katika kiwango chake jukwaani, ingawa katika siku za karibuni ameonyesha kuimarika.

Pamoja na kugoma kutaja jina la dawa anayotumia kwa madai kuwa ni siri yake, lakini mwanamuziki mwenziwe ambaye ni rafiki yake wa karibu alidai kuwa amepatiwa dawa za kienyeji ambazo zinamsaidia kwa kiasi kikubwa ndiyo maana kwa sasa anaendelea vizuri.

Diouf alisema; Mimi siyo Diouf waliyezowea kumwona, nimebadilika kiafya hadi kitabia kutokana na dawa ninayoitumia. Siwezi kuisema dawa iliyonisaidia, siwezi kuitaja na wala sisemi kama ya kienyeji au ya hospitali, atakayekuwa anaihitaji aje anione mwenyewe nitampa siri, lakini wewe sikwambii.

Katika hatua nyingine, raoa huyo alidai kuwa bado bendi hiyo ni imara licha ya kukimbiwa na wasanii kadhaa mahiri akiwemo rapa Chaz Baba aliyejiunga na Mashujaa Musica.

Twanga Pepeta siyo bendi ya msanii mmoja, ina wasanii wengi wenye uwezo mkubwa wa kuimba, akiondoka mtu nafasi yake itazibwa na wasanii wengine waliopo, vijana wenye vipaji ni wengi.

Walikuwepo wasanii wakubwa kama Banza Stone, Ally Choki ambao waliifanyia mambo makubwa Twanga Pepeta kipindi cha nyuma sasa hawapo, na bendi bado inaendelea kufanya vizuri, atakuwa Chaz Baba bana alisema Diouf ambaye pia anapenda kuitwa Sokoine.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms