Thursday, February 23, 2012

..........KASTIFF” KUJENGA KITUO CHA WATOTO YATIMA…........


MSANII wa muziki wa kizazi kipya bongo, Kastiff, amesema kuwa anataka kufungua kituo cha watoto yatima ambacho kitakuwa kinahudumia wale wote wanaishi katika mazingira magumu.

Msanii huyo alitoa kauli hiyo, ambapo alisema kuwa chochote anachokipata katika kazi zake kitasaidia kuwakomboa na wengine ambao hawana uwezo kabisa.

Alisema kuwa hivi sasa yupo katika mchakato wa kutafuta pesa na eneo ambalo atajenga kituo hicho ingawa anawaomba wasanii wengine kumuunga mkono katika mchakato wake huo wa kuwasaidia watoto wa Watanzania.

Alisema watoto wengi ambao wanaishi katika mazingira magumu ni wale ambao wazazi wao wamepoteza maisha kutokana na magonjwa, ajali na vitu vingine vingi.

“Wazazi wakipoteza maisha hali inakuwa ngumu hasa kwa watoto wadogo ambao bado hawajaanza maisha, hivyo katika kuwasaidia kwangu nahitaji kujenga kituo ambacho kitakuwa kinalea watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu,” alisema.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms