Thursday, February 16, 2012

..........IKULU YAFUNGUKA KUHUSU VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA JANA......

Stori kubwa kwenye baadhi ya magazeti ya jana ni kuhusu Rais kikwete kupangua baraza la mawaziri, huku Tanzania Daima ikiandika siku za Waziri wa afya na Naibu wake zinahesabika, Mwakyembe, mwandosya,na chami kupumzishwa.
Hizo stori zimeifanya Ikulu izungumze na AMPLIFAYA ya CLOUDS FM jana na kusema kwamba kazi na wajibu wa kuunda au kubadilisha baraza la mawaziri iko mikononi mwa Rais.
Salva Rweyemamu Mkurugenzi wa habari ikulu alisema “kazi hii sio ya magazeti au vyombo vya habari, inasikitisha sana kwamba kila siku watu wanabashiri tu, baraza lenyewe halibadilishwi japo kila siku magazeti yanaandika hivyo”
Katika sentensi nyingine, Rweyemamu amesema “kuhusu swala la madaktari serikali imeahidi kulimaliza na kweli italimaliza kwa sababu serikali huwa ikiahidi, Inatekeleza kulingana na tarehe waliyopanga na tarehe yenyewe haijafika sasa haraka ya nini, serikali huwa inatekeleza ahadi na watu wote wanajua”
Kuhusu watanzania mbalimbali kuiponda na kuilalamikia serikali kwenye mitandao ya kijamii kwa utendaji mbovu kutokana na mwelekeo wa sasa unaoonyesha mwelekeo mbaya ikiwemo mfumuko wa bei alafu Rais amekaa kimya bila kuzungumza chochote, Rweyemamu alieleza kwamba “serikali haiwezi kuendeshwa na mitandao ya kijamii na wala haiwezi kuzuia watu wasilalamike, Rais ana watu wake hafanyi kazi pekee, lakini pia kuhusu mfumuko wa bei amekua akilizungumzia kwenye hotuba zake mara kwa mara”
Alipotakiwa kutoa neno la mwisho, Rweyemamu amemalizia kwa kusema “Nchi imetulia, inakwenda vizuri, tumuachia Rais afanye kazi yake”

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms