Saturday, February 18, 2012

.........FILAMU YA ‘QUEEN SPEAR’ KUNITAMBULISHA KIMATAIFA ZAIDI….....

MSANII wa filamu bongo Jackline Pantezel, almaarufu kama ‘Jack wa Chuz’, amesema ubunifu aliyouonesha  katika filamu ya ‘Queen Spear‘, ni wa hali ya juu hivyo anaamini itamsaidia kumtoa kimataifa.

Msanii huyo alisema kuwa filamu hiyo ni kati ya anazozitengemea katika kumtangaza zaidi kwani zina matukio mengi ya kusisimua amabyo yamebeba ujumbe za kutosha.

Alisema kuwa anajua amecheza katika kiwango kikubwa lakini anaamini bado kuna makosa machache ambayo yanaweza kuonekana hivyo anahitaji kukosolewa pale ambapo amefanya vibaya.

“Makosa yapo hivyo hatuoni kama yatakuwa ni mengi kiasi kwamba filamu haitafanya vizuri, kazi imetulia na itakuwa moja ya filamu ambazo zitashika kasi baada ya kutoka,” alisema.

Filamu hiyo imetungwa na mtunzi mahiri nchini Aunty Fifii, ambaye ndiye mtunzi wa filamu ya ‘Senior Bachelor’ iliyochukua tuzo ya ZIFF, mara mbili.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms