Sunday, January 29, 2012

......ZITTO KABWE, IDD AZAN NA JOHN MNYIKA, KUSHIRIKI KWENYE FILAMU YA ‘SITAKI DEMU – SINTAH…....

WABUNGE  Zitto Kabwe, Idd Azan na John Mnyika, wanatarajiwa kuonyesha uwezo wao wa kuigiza katika filamu ya ‘Sitaki Demu’ inayoandaliwa na mrembo Sintah a.k.a J’Lo wa bongo.

Sintah alisema filamu hiyo alipanga kuwatumia wasanii  lakini ameona afanye kitu tofauti kwani sasa atawatumia wanasiasa pekee.

Alisema karibia wanasiasa wengi wa hapa nchini watashiriki katika filamu hiyo lakini hao aliowataja ni baadhi ambapo wengine ni mawaziri  pamoja viongozi kadhaa wa Serikali ambao wanapenda michezo.

“Yaani hii filamu itachezwa na wanasiasa pekee, ingawa mwanzo nilitaka kuwashirikisha wasanii lakini nimeona si lazima wacheze kwani kuna watu wengi wenye uwezo wa kuigiza kama hao wanasiasa,” alisema.

Sintah alisema kuwa wasanii wote watakaocheza katika filamu hiyo watalipwa kiasi kikubwa cha pesa hivyo anaamini kazi hiyo itakuwa bora na inaweza kuchukua namba moja kwa ubora kwani itaongozwa watu wenye uwezo mkubwa.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms