Saturday, January 21, 2012

.........WAREMBO WAMKERA MR.CHUZI.........


BAADA ya wasanii wawili Jack wa Chuz na Jini Kabula, kuzichapa kisa kikiwa ni penzi la Mr Chuzi, sasa hali imekuwa mbaya kwao ambapo ‘Chuz’ ameamua kutoa kauli nzito juu yao, na kusema kuwa wakiendelea kumfuatilia atawafikisha kwenye vyombo vya dola.

kwa sasa  Chuzi , aliweka wazi kuwa hana hamu ya kutembea na wasanii hao kwani yaliyomkuta  yanatosha.

Alisema tabia walizonazo warembo hao hazifanani na sura zao hivyo ametoa kauli hiyo ili wakae mbali na penzi lake anamuheshimu sana mke wake.

Hata hivyo  Mr Chuzi, aliwalaumu wasanii hao kwa kufikia hatua ya kutoleana maneno machafu kwa madai ya kutaka kurudiana naye wakati yeye mwenyewe hana hata mawazo hayo.

“Mimi nilisikia kwamba wamepigana kisa penzi langu, kwa hilo nawalaumu sana kwa sababu hawapo kabisa kwenye akili yangu kwanza wanajua nina mke kwa sasa,” alisema.

Aliongeza kuwa endapo wataendelea kumsumbua atawashtaki kwenye vyombo husika kwani wanaweza kuvuruga amani iliyopo ndani ya ndoa yake.

1 comments:

priss said...

ulivyotembea nao

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms