Wednesday, January 18, 2012

........SHILOLE YUKO KWENYE WAKATI MGUMU........

MSANII nyota wa filamu Zena Muhamed ‘Shilole’, yupo katika wakati mgumu kimaisha kwani anadaiwa zaidi ya sh, Milioni 6, kama kodi ya nyumba anayoishi huku akiwa na madeni kwa baadhi ya majirani zake ambapo amepewa muda wa mwezi mmoja awe amelipa pesa hizo.

Msanii huyu anaishi nyumba ya kupanga maeneo ya kinondoni, na inadaiwa kuwa hakulipa kodi kwa muda mrefu kwa kile kinachodaiwa kuwa alikuwa na matatizo ya kifamilia nyumbani kwao Arusha ndiyo maana hakuweza kulipa kodi hiyo.

Akizungumza Jijini Dar, ili kueleza ukweli wa habari hizo Shilole, alisema ni kweli anadaiwa lakini yupo katika mchakato wa kulipa pesa hizo kwani kwa muda mrefu alikuwa akituma pesa nyumbani kwao kwa ajili ya matibabu ya ndugu zake.
Alisema kuwa tangu June mwaka jana hakulipa kiasi cha pesa alichokua akidaiwa hivyo mama mwenye nyumba amempa muda wa mwezi mmoja awe ametoa pesa hizo.

“Jamani ni kweli nadaiwa pesa hizo, lakini nilishindwa kulipa kwani ndugu zangu walikuwa wanaumwa hivyo pesa zote nilizitumia kwa ajili ya matibabu,” alisema.
Hata hivyo aliongeza kuwa baadhi ya majirani zake wanamdai zaidi ya shs laki 7, ambapo hajui atazitoa wapi kipindi hiki ambacho yupo kwenye matatizo kama hayo.

1 comments:

Anonymous said...

badilisha rangi ya baki graundi yako wewe au badilisha rangi ya maandishi unatupa wakati mgumu kusoma habari zako!!

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms