Monday, January 2, 2012

.......MWAKA 2011 ULIKUWA WA MAFANIKIO KWANGU.....

Katika watu wamemaliza mwaka kivingine basi ni mwanamuziki huyu Patcho Mwamba Lukusa “tajiri”.
Kwangu Mimi Patcho mwamba ndio kielelezo cha Msanii kwani ana weza kila sanaa, Patcho Mwamba ni muimbaji, Mtunzi, Composer, Music Arranger, Mchezaji, Mchekeshaji na ni muigizaji pia. Mwaka huu 2011 amemaliza akiwika katika tasmia nzima ya sinema huku ajijizolea umaarufu mwanamuziki huyu toka kundi la FM Academia wana Ngwasuma ameweza kujizolea sifa kem kem toka kwa mashabiki wa Dollywood na wengine hata kuuliza alikuwa wapi siku zote.
Ninachoweza kumhusia tu Patcho Mwamba usije kulewa sifa Uncle fanya kazi Uncle wangu nakukubali sana kimuziki na kiugizaji, na nakwambia utafika mbali. Nimependa Patchou alivyo act kwenye Movie ya Kanumba ambayo imetengenezwa na Kampuni ya Kanumba mwenyewe ya This is IT, jamaa ame act kama ana uzoefu wa miaka kadhaa kwenye industry hii, rafiki yangu Papaa Julie We Estone Le Presidaa Bana Congolee in Tanzania anasema Patchou hakustahili kuwa hapo alipo inawezekana amechelewa kugundua vipaji vyake.

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms