Sunday, January 22, 2012

.......LINAH AJIPANGA KUFYATUA NGOMA MPYA........


LINAH yupo katika hatua za mwisho za kumalizia albamu yake ya kwanza ambayo itakuwa na nyimbo nane.

Binti huyo anayetamba na nyimbo kadhaa zikiwamo Bora Nikimbie, Lonely, Natamani na Nina Furaha, alisema katika baadhi ya nyimbo za albamu hiyo atawashirikisha baadhi ya wasanii nyota.

Msanii huyo ambaye anashikilia tuzo mbili za muziki za Kilimanjaro za mwaka 2011 za Msanii Bora wa Kike na ile ya Msanii Anayechipukia, alisema kazi aliyoifanya katika albamu yake hiyo ndiyo ambayo itaonyesha tofauti yake na wasanii wengine.

Alisema kukubaliwa kwa kazi zake za awali ndiyo kitu ambacho kimemsukuma kuandaa albamu hiyo ambayo alisema ni mapema mno kuitaja jina.

Unajua ukiona hata watoto wanaimba nyimbo zako, jua tayari umetoka,alisema na kuongeza kuwa baada ya uzinduzi ziara ya mikoani itafuata.

Amewamwagia sifa wasanii wenzake wa Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT) kwa sapoti wanayompa.

Pale kuna watu kama Barnaba na Amin, kuna wakati wao walitunga na kunipa nyimbo niimbe. Lakini katika albamu ninayoiandaa, nyimbo zote nimetunga mwenyewe, alisema.

1 comments:

priss said...

uko juu , ila jifunze kuvaa ndo umevaa nini top ya elfu 7 kariakoo

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms