Saturday, January 21, 2012

.......KENNY KUFUNGA NDOA MWAKA HUU......


Kenny Victor ‘Kenny’, amesema kuwa anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi Miriam Gerald, ambaye alikuwa Miss Tanzania 2009/2010, ambayo itafungwa June mwaka huu.

Kenny na Miriam walianza mahusiano ya kimapenzi tangu mwaka 2008 na hadi sasa tayari wana mtoto mmoja ambaye amepatikana baada ya mrembo huyo kuuvua U-miss.

Mwaka jana wawili hao walitangaza kufunga ndoa, lakini haikuweza kufungwa ambapo,  
Kenny ameamua kutoa kauli ya mwisho kuwa watafunga ndoa hiyo June mwaka huu.

Akizungumza mwandishi wa habari hii,
Kenny alisema kuwa anaamini baada ya kuisubiri kwa muda mrefu ndoa yake sasa kila kitu kimekamilika na kinachosubiriwa ni siku hiyo iweze kufika.

Aliongeza kuwa hivi sasa yuko Mwanza ambapo ameenda kwa ajili ya kulea mtoto wake ambaye naye anaweza kuwa msanii au atajihusisha na mambo ya urembo.

“Kwa sasa nipo Mwanza nalea kidogo na kama unavyojua mwaka jana ilibidi tufunge ndoa lakini kutokana na sababu fulani hatukuweza kufanya hivyo, ila mwaka huu kila kitu kinaenda sawa na ndoa yetu itafungwa mwezi June mwaka huu,” alisema.

1 comments:

priss said...

honereni mleeeni mtoto ewnu katika maadili mema nawatakia mafanikio mema

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms