Monday, January 16, 2012

........DON'T MISS THIS, PLEASE READ IT..........


Kwa kudra za mwenyezi mungu naamini kuwa wadau wetu wote wa blog hii mu wazima wa afya, na zaidi ya yote naamini kuwa sote tunaendelea vyema na ujenzi wa taifa letu (Tanzania).

Pia ningependa wadau wa blog hii mtambue kuwa mimi binafsi nawapenda na kuwajali nyoteee, nasema hivi HAKUNAGA mtu muhimu kwangu kama mdau wa blog hii.

Ningependa kuchukua nafasi hii kuwaarifu kuwa kwasasa blogger wenu mtiifu niko nje ya nchi ya Tanzania, so kwa yeyote ambaye angependa kuwasiliana na mimi itabidi atume email na asitumie namba yangu ya simu cz I am not reachable. Hali kadhalika mtaniwia radhi kwa kuchelewa kuwarushia habari kwa wakati. Actually the main reason ni kwamba  huku nilipo majira yanapishana sana na ya Bongo. Lakini naomba niwahakikishie kuwa burudani zitaendelea kuwashukia kama kawaida. Nitajityuni niwe naamka usiku wa manane ili niweze kuwalete habari kwa wakati.

Jamani mpoooooo?????  Nawapendaga wote mjue……. Hata hivyo ningependa mjue kuwa  nahuzunishwa sana na baadhi ya wadau wanaonitumia email wakiwa wameandika meseji za kutukana, ndugu zangu ustaraabu ni kitu muhimu sana. Kama unadhani kuna kitu nimeenda kinyume nipe ushauri name nitaupokea, kwani binadamu tunajifunza kutokana na makosa.

Pia ningependa kuchukua fursa hii kuwataarifu kuwa kuna baadhi ya Wataanzania vijana wanajitahidi sana kufanya shughuli za kujitolea kwa ajili ya kusaidia Watanzania wenzetu wasiokuwa na uwezo. Kwa kutambua hilo na sisi wajanja blog kuanzia mwezi wa pili tutaanza kutoa makala zinazohusu vijana hawa wanaojitoa kwa ajili ya jamii na tutaelezea bayana shughuli wanazozifanya.
Kwa kutambua hilo kuanzia mwaka huu wa 2012 mapato yote yatakayopatikana kwenye blog hii asilimia 60 ya mapato hayo  yataenda moja kwa moja kusaidia watoto yatima….. Tunaomba tuwaunge mkono watanzania wenzetu wanaojitoa kwa ajili ya kusaidia wengine. Mwishoni wa mwezi huu tutawaambia sehemu ambapo mapato ya blog hii yanaenda kwa lengo la kusaidi watoto yatima.

Asanteni sana na mungu awabariki nyoteeeeee

MUNGU IBARIKI TANZANIA , MUNGU IBARIKI AFRIKA

2 comments:

Anonymous said...

hatuwezi kusoma yELLOW can u pls change this

priss said...

hivi mtu ukituma coments zako zinakaa baada ya muda gani ili watu wengine wasome?????

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms