Thursday, November 24, 2011

........MZEE CHILO ATOA SOMO KWQA WASANII WENZAKE.....

Mkongwe wa sanaa ya uigizaji Tanzania, Ahmed Olotu Mzee Chilo amedai kuwa katika fani hiyo kwa sasa kuna mabadiliko makubwa ya kutojali maadili tofauti na ilivyokuwa awali.
Chilo ambaye alitamba zaidi alipokuwa akiigiza tamthilia ya Jumba la Dhahabu, ametoa kauli hiyo kutokana na vitendo vilivyoongezeka kama kukumbatiana na mavazi yasiyo ya kistaarabu ambavyo awali havikuwepo.
Amesema: Sanaa ya uigizaji kwa sasa ina mabadiliko makubwa hasa katika suala la maadili, kuna mambo sasa yamekuwa fasheni.
Katika uigizaji sasa watu wanakumbatiana, lakini pia wanavaa mavazi mafupi ambayo kwa mzee wa zamani akiona, lazima ashangae.
Mbali na Jumba la Dhahabu, Mzee Chilo amecheza filamu za Miss Bongo, Vita vya Ushindi, Cross My Sin, Tanzia, My Heat Copy, Utata, Silent Killer, Never Forget You, Diversion of Love na Engagement Day.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms