Wanamuziki watakaotumbuza kwenye tamasha la Tusker All Stars 2011 ambalo linatarajiwa kufanyika Oktoba 1 kwenye viwanja vya Canirvo,leo mapema wameshiriki kwenye zoezi la upandaji miti kwenye msitu wa Karura (Karura Forest),nje kidogo ya jiji la Nairobi,Nchini Kenya.Zoezi hilo limefanyika pia likiwa ni maalum ya sehemu ya kumuenzi aliyekuwa mwanaharakati mahiri wa mazingira nchini Kenya ambaye kwa sasa ni marehemu,Prof.wangari maathai wa nchini humo.
Mwanamuziki mahiri kutoka nchini Marekani,Shaggy Akipanda Mti
Wanamuziki watakaotumbuiza kwenye tamasha la Tusker All Stars 2011 Oktoba 1 kwenye uwanja wa Carnivo, Shaggy,Cabo Snoop,Davis,Alpha,Peter Msechu wakishirikia na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya EABL,Kenya,wakiongozwa na Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo Caroline Ndugu wameshiriki zoezi la upandaji miti mapema leo asubuhi kwenye msitu wa hifadhi ya miti uitwao Karura Forest kwa ajili ya kuihamasisha jamii katika suala zima la kulinda na kuhifadhi mazingira,aidha pia zoezi hilo limefanyika ikiwa ni sehemu ya kumuenzi Mwanaharakati wa Mazingira,Prof Wangari Maathai,ambaye amefariki hivi karibuni jijini Nairobi,nchini Kenya.
Mwanamuziki mahiri kutoka nchini Marekani,Shaggy akimwagilia maji mti wake alioupanda mapema leo asubuhi kwenye msitu wa hifadhi ya miti,Karura Forest,ilioko nje kidogo ya jiji la Nairobi nchini Kenya.Zoezi hilo la upandaji miti limeratibiwa na kampuni East African Breweries Ltd,Kenya kwa madhumuni ya kumuenzi mwanaharakati wa mazingira nchini humo,Prof.Wangari Maathai.Kulia ni Mkurugenzi wa masoko EABL-Kenya,Caroline Ndugu na pichani kati toka kulia ni Msanii Cabo Snoop kutoka nchini Angola.
0 comments:
Post a Comment