Friday, July 1, 2011

.......H.BABA NA MCHUMBA WAKE FLORA MVUNGI KUKIMBIZA NA FILAMU YAO YA TRAFIC PORI........


FILAMU kali na ya kusisimua Trafic Pori inatarajiwa kuletwa na Nyota wawili ambao kwa sasa ni wachumba, filamu hii iliyotungwa na Muigizaji na mwanamuziki mahiri wa muziki wa Bongo Fleva Bolingo Hamis Ramadhan Baba almaarufu kama H. Baba, inamshirikisha Nyota wa filamu hapa nchini Frola Mvungi ambaye ni Mchumba wa H.Baba, msanii huyu akiongea na FC amesema kuwa filamu hii ni hadithi inayoelezea maisha kwa ujumla na ni hadithi ya kipekee.
“Kwa kifupi filamu ipo tayari kila kitu, bali kuna mambo ambayo tunayasubiri kutoka upande wa pili yaani kutoka kwa Msambazaji wa filamu, humo bwana kuna waigizaji wakali kibao huku jahazi likishikwa na mimi mwenyewe na mama Frola, ni hatari si filamu ya kitoto bali ni moto wa kuotea mbali, maana unakutana na vipaji vya ukweli katika filamu ya ukweli” Anasema H. Baba.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms