Saturday, October 6, 2012

.....SASA NATINGA KWENYE UANDAAJI WA FILAMU RASMI.....

MTAYARISHAJI na mwigizaji wa filamu za Bongo, Dometria Alphonce 'DD', ameingia rasmi katika uandaaji wa filamu kwa kuandaa filamu inayohusu maisha yake halisi ya ndoa.

Msanii huyo ameamua kurekodi filamu hiyo inayoitwa 'Kua Uyaone' kama faraja kwa wanawake wanaokutwa na misukosuko katika ndoa zao.

"Filamu ya Kua Uyaone ni filamu yangu ya kwanza kuandaa na kuigiza nikiwa mhusika mkuu. Inazungumzia maisha yangu halisi ya ndoa," alisema.
"Inaonyesha jinsi nilivyoteseka na kumpoteza mume, nimefanya hivi ili kuwatia nguvu wanawake wenzangu."

Dometria ambaye ni pacha wa msanii wa filamu nchini Dotnata, anasema kuwa amekuwa akiandika hadithi za filamu kwa muda mrefu, lakini alikuwa akishiriki sehemu fupi fupi tu za filamu zilizoandaliwa na pacha wake huyo ambaye ni Doto.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms