Monday, October 8, 2012

....AFANDE SELE ALONGA......NI BALAA TUPU.....WAKATI muziki Hip Hop ukizidi kushika kasi, msanii kutoka mji kasoro bahari Morogoro, Afande Sele au unaweza kumuita King of Rhymes, amesema kuwa kuna baadhi ya watu ambao wanajiita wadau wa muziki walitaka kuua muziki wa Hip Hop ili kuwapa nafasi wabana pua lakini walishindwa kutokana na halikati zao na hakuna kilichofanyika.

Msanii huyo aliwafumbua macho mashabiki wao kuwa muziki huo unaozungumza maisha halisi ya mwanadamu kunanbaadhi ya watangazaji na wadau ambao lengo lao lilikuwa ni kuuzimisha muziki huo baada ya kuona ujumbe unaopatikana una lengo la kuelemisha zaidi jamii na si wale wanaoimba ujumbe wa mapenzi tu.

Alidai kuwa muziki wa Hip Hop haujapewa nafasi kama ilivyo kwa wabana pua na ndiyo maana hata vijana wengi wanashindwa kujua nchi inakwenda wapi kutokana na nyimbo za mapenzi kushika kasi kila siku.

“Unajua kuna watu wanajifanya wadau wa muziki wakati lengo lao ni kuua muziki wa Hip Hop na kuwapa nafasi waimba mapenzi lakini hata hivyo bado muziki wetu utazidi kuwa juu kutokana na ujumbe unatolea ndani ni ule wa kudumu miaka mia lakini mapenzi leo na kesho wimbo hauna tena maana,” alisema Afande.


0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms