Friday, October 5, 2012

......NABADILISHA MWENENDO.......


MWIGIZAJI wa kike katika tasnia ya filamu za Swahiliwood, Leanatha John 'Semera', ameamua kubadili uelekeo kutoka kuigiza sana tamthilia na kuelekeza nguvu katika filamu.

Msanii huyo anaamini kuwa anapokuwa katika filamu ni rahisi kung'ara.

"Nimeigiza sana katika tamthilia na nilikuwa katika tamthilia ya Millosiss chini ya uongozi wa Mr. Chuzi, pia nimeshiriki filamu kadhaa na sasa nimejiunga katika kampuni mpya na tayari nimeanza kurekodi filamu ambayo itaingia sokoni hivi karibuni," alisema Semera.

Kipaji cha msanii huyo kilivumbuliwa na Mr. Chuzi na sasa amekuwa ni msanii mkubwa anayefanya vizuri katika tasnia ya filamu.

Mkurugenzi wa SSG Production, Mshindo Jumanne, alisema msanii huyo uwezo wake ni mkubwa na atawafunika nyota wa filamu Bongo.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms