Wednesday, October 10, 2012

........KWENYE FILAMU ZA BONGO HUWEZI KUYAKOSA MAMBO HAYA.....


KWA Nigeria ambako ndiko kumeendelea zaidi kwa sasa katika suala la filamu barani Afrika, walianza na filamu zilizojikita katika uchawi na nguvu ya dini dhidi ya imani hizo za giza.

Baadaye wakaingia katika jamii, wakizungumzia uhusiano na usaliti katika ndoa na mambo mengine.

Hiyo kwao ilikuwa ni alama au utambulisho mkubwa vikiwa na lafudhi ya kikwao katika kuzungumza Kiingereza. Kupitia filamu zao huwezi kushindwa kubaini kuwa hawa ni waigizaji kutoka Nigeria.

Kwa upande wa filamu za Bongo, kuna mambo kadhaa ambayo ukiyaona lazima ujue kwamba hiyo ni filamu ya Kibongo. Huwezi kuyakuta mambo hayo kwa waigizaji wa sehemu nyingine.

Shuka nayo.

1. Jini likifika barabarani kabla ya kuvuka linaangalia pande zote kushoto na kulia kisha linavuka barabara. Sijui kama ni sahihi.

Maana inasemekana kuwa jini ni kiumbe chenye miujiza na uwezo mkubwa katika kutenda mambo yake hata kama kiumbe hicho kitajibadilisha kuwa katika umbo la binadamu, lakini uwezo wake unabaki pale pale.

Sasa huyo jini anayeogopa magari katika kuvuka barabara ni jini gani?

2. Matajiri wetu katika filamu majumba yao yana askari badala ya mageti yanayotumia umeme. Lakini jambo linaloshangaza zaidi ni walinzi hao, mara nyingi hutambulishwa kwa utaahira au wachekeshaji huku wakivalishwa uhusika wa kupenda masihara yanayokera. Mlinzi anakuwaje mwendawazimu?

3. Utangulizi (Trailer) wa filamu inachukua hadi dakika 40.

4. Baada ya kutuunganishia Sehemu ya 1 na 2 ambazo ndio zimepewa jina la Part 1 na Part 2, ukiangalia filamu ya Part 2 mwanzo tu unajua Part 1 ilikuwaje.

Hapa watazamaji wanahisi kuibiwa, maana yake ni kama daladala linalotoka Kariakoo kwenda Kimara, halafu baada ya kufika Magomeni abiria wanaambiwa litaishia Manzese ili kutoka hapo alipe tena nauli mpya kwenda Kimara. Jamani safari moja nauli mara mbili?

5. Mademu wanaonekana wakiamka asubuhi wakiwa wamepambwa kabisa (make-ups) usoni na hereni. Hii inaonyesha kuwa katika filamu zetu hakuna kulala wala kugonga msosi. Haya nayo ni maajabu.

6. Waigizaji wa Bongo wakifika hotelini imezoeleka kuona wakiagiza juisi au mvinyo isiyofunguliwa. Nadhani bajeti ya utengenezaji filamu ni ndogo jambo linalofanya maigizo yazidi katika filamu zetu na watazamaji kugundua ubovu.

7. Nusu saa mwigizaji anatembea, anafanya mazoezi, anakimbizwa mara ananunua vitu.

8. Wimbo wa malavidavi unaimba mpaka unaisha, hili ni katika filamu za Bongo Movie lakini filamu za wenzetu ni nadra kutokea.

9. Msanii yupo kijijini, maisha ni magumu lakini kichwani nywele zimepakwa dawa na zinameremeta kwa mafuta. Kweli inaonyesha jinsi gani wasanii hao wanavyojipenda, lakini kwa mtu anayewakilisha maisha magumu ya kijijini anapaswa kuwa hivyo?

10.Wote wanaouawa kwa bunduki hupigwa kifuani au tumboni. Huwezi kuona sehemu nyingine. Au bunduki za Bongo zinachagua?

11.Jambazi lazima awe anavaa miwani nyeusi, koti jeusi na mvuta sigara. Hivi kumbe wahalifu wote wa Bongo au duniani wana tabia zinazolandana?

12. Mtu akiigiza tajiri lazima anakuja kumpenda masikini, watu hawa wanakutana wapi au ndiyo maisha halisi?
Hayo ndiyo matukio yanayojiri katika filamu za Bongo ambayo yanafanya mashabiki wajiulize kama kweli tupo makini na biashara au tunalipua.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms