Thursday, September 6, 2012

......PICHA YA AKI YAZUA MASWALI MENGI.....

WIKI hii katika mitandao kadhaa ya Nigeria imesambazwa picha za mwigizaji Chinedu Ikedieze 'Aki' akiwa amemkumbatia mtoto na kuzuka habari kuwa nyota huyo wa filamu za Nigeria alipata mtoto kabla ya kuoa.

Habari zimezagaa kuwa Aki amekuwa akificha ukweli kuhusu mtoto wake ingawa taarifa za ndani zinasema kwamba mkewe aitwaye Nneoma anafahamu juu ya jambo hilo.

Hata hivyo, Aki hakutaka kutoa ufafanuzi juu ya mtoto huyo kwa madai kwamba hayo ni maisha yake binafsi.
Aki na Nneoma walifunga ndoa mwaka jana.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms