Wednesday, August 15, 2012

.....SASA NAANZA KUANDAA FILAMU ZANGU MWENYEWE.......

RAMSEY ameingia rasmi katika uandaaji wa filamu baada ya kushiriki kazi za watayarishaji wengine kwa muda mrefu.

Msanii huyo anasema sasa ana zaidi ya filamu 120 alizoshiriki kuigiza lakini hakuna hata filamu yake moja.

Mwenyewe naweza kuandaa filamu yangu baada ya kutumiwa sana na wenzangu ni ushindi na furaha pia," alisema.

"Filamu ya Binti Yangu ni filamu yangu ya kwanza kabisa katika maisha yangu kutengeneza mwenyewe, ni ushindi na ninawatia moyo wasanii wengine kujaribu."

Anasema kuwa unapokuwa na filamu yako ambayo unashiriki, kila ulichopanga huenda kama unavyotaka kwa mantiki hiyo ni tofauti na filamu unayoshirikishwa kuna wakati unashindwa hata kuchangia kwani wengine hawapendi ushauri.

Katika filamu hiyo anawashirikisha wasanii wakali katika tasnia ya filamu kama Grace Mapunda, Lucy Komba, Mohamed Funga Funga Mzee Jengua, Heriety Chumila, Diana Exavery, Jennifer Raymond Penina, Jumanne Mshindo, Ramsey mwenyewe na wengineo.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms