Thursday, August 16, 2012

.......JASMINI NI TISHIO KWA WOLPER......

MWIGIZAJI wa kike anayekuja kwa kasi katika tasnia ya filamu za Swahiliwood, Neema Oberlin Kimaro 'Jasmin', ndiye tishio jipya kwa msanii anayengara kwa sasa, Jaqueline Wolper Massawe.

Neema mbali ya kuwa ni msanii anayetoka Kilimanjaro anakotoka pia Wolper, kwa muda mfupi tangu aingie katika tasnia ya filamu ameonyesha uwezo mkubwa hasa katika filamu ya Essau.

"Tangu nianze kuigiza, watayarishaji wananikubali na kuniambia uwezo wangu ni mkubwa na ninaweza kabisa kumpoteza Wolper ambaye pia kwangu ni moja kati ya wasanii wanaonivutia," alisema Neema anayevutiwa pia na Monalisa na Johari.

"Nipo kikazi zaidi na sihofii ushindani, bali siku ya siku mimi ndiye natarajia kuwa mshindi."

Mtayarishaji wa Essau, Mshindo Jumanne, alimsifu msanii huyo hasa kwa kuchambua ushiriki wake katika filamu hiyo alipocheza nafasi ya mhusika mkuu alipoigiza kwa kutumia jina la Jasmin.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms