Wednesday, July 4, 2012

......WA-NIGERIA HAWAZIJUI FILAMU ZA KIBONGO.....

MWIGIZAJI maarufu kutoka nchini Nigeria Omotola Jalade amesema kuwa filamu za kitanzania hazipo katika soko la filamu nchini kwao wala hawazijui.

Mwigizaji huyo aliyekuwa Bongo hivi karibuni alisema, pamoja na kuwa wao wanajulikana zaidi Afrika Mashariki lakini ukweli ni kwamba nchini kwao bado hawajaitambua Tanzania hususani katika suala zima la sanaa hiyo ya filamu.

Nilichowahi kusikia kuhusu Tanzania ni msiba wa msanii mmoja mkubwa wa filamu, lakini si vinginevyo alisema Omotola na kuongeza kuwa ili Tanzania ifike juu katika tasnia ya filamu, serikali inatakiwa kufanya juhudi za makusudi kufungua milango kwa ajili ya filamu za kitanzania.

"Njia kama hiyo ilitumiwa na Nigeria na ndio maana leo hii filamu imekuwa chanzo kizuri cha mapato sio tu kwa wasanii binafsi bali hata kwa taifa kwa ujumla. Juhudi za mtu mmoja mmoja haziwezi kuzaa matunda ikiwa serikali yenu itakaa pembeni katika hili. Hivyo ni lazima iweke mkono wake. Hii itasaidia kuleta maendeleo ya kweli," alisema

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms