Thursday, July 19, 2012

.............SITEMBEI NA MUME WA MTU........

BINTI mrembo ambaye ni mwigizaji wa Nollywood, Lizzy Anjorin amekanusha habari zilizoenea kwamba ana uhusiano wa kimapenzi na mume wa staa mwenzie Funke Akindele.

Msanii huyo alidai kuwa tuhuma hizo zimemdhalilisha na anaangalia uwezekano wa kuyashtaki magazeti yaliyomtuhumu na kumshushia heshima. Habari hizo zilienezwa kwenye mitandao mingi ya kijamii nchini Nigeria na Ghana wiki moja iliyopita.

Msanii huyo aliyefungua Supamaketi mpya jijini Lagos, alisema; "Hii inanishangaza sana, nashangaa kwanini watu hawataki kuniacha na maisha yangu, simjui hata huyo mume wa Funke na wala sijawahi hata kumpitia karibu sehemu yoyote ile."

"Wala kwenye harusi yao sikwenda wala sina hata namba zake. Nimechoka sasa inabidi nichukue hatua za kisheria zaidi, nataka waniache na maisha yangu, wasieneze mambo ambayo si ya kweli kwa jamii," alicharuka Lizzy.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms