Tuesday, July 17, 2012

........NIMWIGE JOTI KWA LIPI?????.......


MSANII wa vichekesho Swahiliwood, Ali Juma Master face kutoka Kundi la Ze Comedy ambalo hurusha vichekesho vyake katika televisheni ya EATV, amekanusha vikali kuwa yeye uhusika wake anamwiga sana msanii mwenzake kutoka Kundi la Orijino Komedi, Joti kwa kila jambo analolifanya.

Mimi siwezi kumwiga Joti kuigiza kwa sababu wote tupo hapa hapa au siyo? Mimi naigiza kama Master face na siigizi kama msanii mwingine anayeigiza kama mimi, lakini naweza kusema kuwa ninaikubali kazi yake ni nzuri, yeye ana watu wake na mimi nina watazamaji wangu, labda useme kuwa kijana anajitaidi kuleta upinzani kidogo kwangu,anasema Master face.

Master face amekuwa akiigiza na kurandana na msanii nyota katika uchekeshaji, Joti kwa kufanana kwa vitu vingi, lakini Master face alikiri kuwa katika ya watu walimvutia na kuingia katika uchekeshaji ni Mr. Ben, marehemu Max huku akisema uigizaji wa Joti upo katika damu yake na ndio hasa msanii anayemkubali na kuwa ni mwongozo wake.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms