Friday, July 6, 2012

.......MISS SINZA HIYOOOOO...


JUMLA ya warembo 15 wamejitokeza kuwania taji la Mrembo wa Sinza Redds Miss Sinza 2012 katika shindano litakalofanyika Julai 13 kwenye ukumbi wa Mawela social (Ten Star Lounge) uliopo karibu na hoteli ya Vatican City.

Mratibu wa mashindano hayo, Majuto Omary wa kampuni ya Calapy Entertainment aliwataja warembo hao kuwa ni Mariam Miraji, Naima Mohamed, Lulu Ambonela, Maria John, Eva Mushi, Vailet John, Esther Mussa, Christina Samwel, Nahma Said, Shadya Ali, Aisha Ramadhan, Nancy Musharuzi, Brigitter Alfred na Merina Mushi.

Majuto alisema kuwa warembo hao wapo kambini chini ya mwalimu wao, Mwajabu Juma ambaye kwa sasa anashikilia taji la Miss Tanzania Top Model.
Alisema kuwa mazoezi ya warembo hao yanafanyika kwenye ukumbi wa mashindano hayo, Mawela social kuanzia saa 8.30 mchana.

Warembo wamepania kufanya kitu cha kihistoria siku ya shindano na hii inatokana na ukweli kuwa wamejiandaa vilivyo na hivi sasa wanamalizia tu baadhi ya vitu vidogo vidogo vya mashindano hayo," alisema Majuto.

Alisema kuwa lengo kubwa la mashindano ya mwaka huu ni kutwaa taji la Redds Miss Tanzania mbali ya taji la Kanda ya Kinondoni katika shindano hilo lililodhaminiwa na Redds Premium Cold, Dodoma Wine, Kidoti Fashion, Clouds Entertainment, sufianimafoto.blogspot.com, Lady Pepeta na flexi P, Fredito Entertainment, Screen Masters, Brake Point na Jackz Cosmetics Kinondoni.

Tuna warembo moto wa kuotea mbali ambao kwa sasa wameonyesha kupania kufanya kile ambacho kimesubiriwa na wadau wa warembo wa mitaa ya Sinza na vitongoji vyake, hii inatokana na ukweli kuwa mashindano haya ni ya mwisho kwa upande wa vitongoji jijini, alisema.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms