Monday, July 30, 2012

........LADY GAGA AJIVIKA UMALIKIA.....

TANGU alipokutana na Malkia Elizaberth II wa Uingereza mwezi uliopita, Lady Gaga, amejinunulia taji (crown) ambalo hujivalisha na kujiita mtawala.

Baada ya kukutana na malkia huyo, Lady Gaga alikwenda moja kwa moja kwa mbunifu wa Louis Vuitton na kumtaka amtengenezee taji.

Alitakiwa kuchagua aina ya taji ambalo angependa kutengenezewa na baada ya kufanya hivyo alitakiwa kulipa kiasi cha dola za Marekani 30,000. Alilipa mara moja.

Sasa hivi anavaa taji hilo anapokuwa nyumbani, lakini watu wake wa karibu wanasema anajizoesha kabla ya kuanza kutoka nalo nje.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms