Tuesday, July 17, 2012

......FILAMU ZETU BADO HAZIJAKAA VIZURI - PASTOR MYAMBA.......

MUIGIZAJI wa filamu za Bongo, Pastor Myamba amesema filamu nyingi za Tanzania zinakosa weledi katika uandishi, uongozaji, uhariri na hata uumbaji wa wahusika.

"Lazima tukubali udhaifu huu turekebishe, nimekuwa katika tasnia ya filamu kwa muda mrefu sasa lakini kuna changamoto nyingi katika tasnia ya filamu, na jambo ambalo nimeliona ni wasanii kukosa ujuzi kitaaluma katika utendaji wa filamu kwa ujumla, kwa mantiki hiyo nikaamua kufungua chuo hiki kwa ajili ya wasanii maskini wasio na uwezo wa kulipa ada kubwa katika vyuo vilivyopo, lakini pia kutoa nafasi kwa wale ambao wanafanya kazi lakini taaluma imekuwa shida kwao, na mwito ni mkubwa kweli.

Tatizo la wasanii wa Tanzania kushindwa kufaidika na vipaji na ujuzi wao, ni kukosa elimu ya kutosha ya mambo ya sanaa, kwa mantiki hiyo nikaamua kufungua chuo hiki kwa ajili ya wasanii, nimeapa kwamba nitaweka ada ndogo ili wasanii wachanga au kwa ujumla tuseme wasio na uwezo mkubwa wa fedha waweze kusoma hapa.

"Nina imani kuwa kusaka maarifa ya namna ya kutengeneza sinema zenye uhalisia na visa litasaidia kuleta ushindani sio tu wa ndani bali wa kimataifa.

Ikumbukwe kuwa filamu ambazo zinakosa uhalisia zinapunguza mvuto, na hivyo kuwafanya watazamaji kuishiwa na hamu ya kuziangalia filamu hizo na kuwakosesha kipato na kuongeza umasikini miongoni mwa wasanii.

Pia wasanii na watendaji wengine wanapaswa kupatiwa mafunzo, kwangu mafunzo ndiyo kitu cha kwanza muhimu kwa mtu yeyote yule katika kumuongezea stadi zake za utendaji. Kwa jumla kuna upungufu mkubwa wa mafunzo ya fani mbalimbali za sanaa, ikiwemo filamu.

"Wasanii wengi wanajifunza kwa kuiga wenzao. Ingawa hii ni moja ya njia za kujifunza, tatizo lake ni kuwa huchukua muda mrefu na haina hakika kama kinachoigwa ni sahihi au la," alisema.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms