Tuesday, July 3, 2012

..........DOGO JANJA HAKIELEWEKI......

WIKI mbili zilizopita msanii Dogo Janja alijitoa katika kundi la Tip Top Connection na kurudi kwao Arusha kwa basi, lakini sasa amerejea Dar es Salaam kwa ndege na kusaini mkataba na kundi la Watanashati linaloongozwa na Ostaz Juma.

Lakini katika hali ya kushangaza, meneja wake mpya huyo tayari ametangaza kuwa yeyote ambaye yupo tayari kumchukua kijana huyo anaweza kufanya hivyo. Kauli ya Ostaz Juma imezua maswali.

Dogo Janja alipokewa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wikiendi iliyopita na wadau lukuki wa muziki wa kizazi kipya.

Mapokezi yake hata hivyo yameibua maswali kuhusiana na hatua ya wazazi wa kijana huyo kumwachia bila ya uangalizi maalum.

"Unajua japokuwa watu wengi wamesema kuwa mimi nilikosea, lakini hawajui lolote. Ninayejua ni mimi mtendwa, wengi walikariri yaliyosemwa na Tip Top kuwa mimi nilikuwa mtoro, mkaidi," alisema Dogo Janja akiwa uwanjani hapo.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms