Wednesday, June 27, 2012

.......WAREMBO WA MISS UNIVERSE TANZANIA 2012 WAANZA KAMBI RASMI…...Warembo wa Miss Universe Tanzania 2012 wameanza rasmi kambi katika hoteli yenye hadhi ya kipekee Urban Rose Hotel. Hii ni kwaajili ya kujiandaa na fainali ya Miss Universe Tanzania 2012 itakayofanyika tarehe 29 mwezi huu wa juni. Miss Universe Tanzania pia imeandaa mafunzo mbalimbali kwa ajili ya kuwapa warembo ili kujitambua kama vijana na kama wanawake. Mafunzo hayo yatakuwa yakitolewa na wataalamu mbalimbali toka katika nyanja tofauti ikiwemo TGNP.

Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications ambaye pia ni mkurugenzi na muandaaji mkuu wa kitaifa wa mashindano haya Maria Sarungi Tsehai amesema kuwa tofauti na miaka ya nyuma mbali na kuongeza semina zaidi ili kuwasaidia warembo lakini pia imefanikiwa kuongeza mikoa ambapo mwaka huu wameshiriki warembo kutoka mikoa saba ya Tanzania.

Mbali na kutafuta warembo tu bali Miss Universe ni kama chuo cha kufundisha warembo juu ya kujitambua kama mwanamke na kumpa mbinu mbalimbali za kimaisha.Vilevile mbali na mshindi kupata nafasi ya kutembea nchi mbalimbali za kimataifa pia hutoa fursa kwa mshindi kupata nafasi ya kwenda kusoma nje ya nchi kama vile Marekani kwa kupitia mdhamini wetu mkuu New York Film Academy Kambi ya Miss universe Tanzania 2012 imekamilishwa na warembo 20 kutoka mikoa saba ya Tanzania ambayo ni Dodoma, Arusha, Mwanza, Kilimanjaro, Manyara, Mtwara na Dar es Salaam.

Mashindano ya Miss Universe Tanzania yalianza rasmi mwaka 2007 ambapo mrembo wake wa kwanza alikuwa ni Flaviana Matata ambaye mbali na kuliletea sifa taifa bali pia amepata mafanikio makubwa katika fani ya ulimbwende kwa kuwa mwanamitindo wa kimataifa. 2008 Miss Universe Tanzania iliwakilishwa na Amanda Ole sululu, 2009 Illuminata James, 2010 Hellen Dausen na Nelly Kamwelu ambaye ndiye anakabidhi taji kwa mshindi wa mwaka huu.

Mashindano ya Miss Universe Tanzania yamedhaminiwa na Le Grande Casino, The citizen,Urban Rose Hotel, Amina Designs, Dodoma Hotel na New York Film Academy. (Kwa hisahi ya KajunaSon)

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms