Monday, June 25, 2012

....VYOMBO VY HABARI VYAMKERA CHRIS BROWN.....


STAA Chris Brown amesema vyombo vya habari vimekuwa vikipotosha ukweli kuhusu ugomvi uliotokea hivi karibuni kati yake na rapa Drake.

Brown alisema vyombo vya habari vimekuwa vikielemea upande mmoja bila kutaka kuchunguza ukweli wa ugomvi huo.

"Ninasikitishwa na jinsi vyombo vya habari vinavyoripoti hili jambo, hakuna anayejua ukweli wa ugomvi ule zaidi yangu mimi na Drake, kwanini hamuulizi mnaandika tu?" Alihoji Brown katika mtandao wa twitter.

Pamoja na kuvilaumu vyombo hivyo, pia anamtupia lawama, Drake, kuwa ndiye aliyeanzisha ugomvi huo kwa kurusha chupa hewani.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms