Monday, June 25, 2012

....ULEVI NOMAAAAA......


AMA kweli pombe si chai. Mwanamuziki mtaratibu, Adele, anasema hata yeye aliwahi kutendwa na ulevi katika moja ya shoo zake huko Uingereza.

Adele anasema siku hiyo 'alipiga maji' kisawasawa wakati alikuwa na shoo, kilichomtokea siku hiyo hatakisahau maishani mwake.

Kama kawaida, alipanda jukwaani kuanza kuimba, akiwa amekaa kwenye kiti ghafla alidondoka mpaka chini na kuwapa kibarua wasaidizi wake kumnyanyua.

Lakini hiyo ilikuwa tisa, kumi ni pale alipojaribu kuendelea kuimba na kujikuta hana kumbukumbu ya mashairi ya wimbo unaopigwa.

"Ilikuwa ni aibu ya mwaka. Kwanza nilidondoka mpaka chini, pili nikasahau mashairi ya wimbo wangu mwenyewe," anasema Adele.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms