Thursday, June 14, 2012

....UJAUZITO UMEPUNGUZA KASI YANGU KWENYE TASNIA YA FILAMU.....


MWADADA mwigizaji wa filamu za Swahiliwood, Maua Kassim, amekiri ujauzito alionao umepunguza kasi yake ya uigizaji kwa kiasi kikubwa kwani mara nyingi anajihisi uchovu.

Msanii huyo ambaye ameshiriki katika filamu na wasanii mahiri, anasema alikuwa anaandaa kipindi chake kwa ajili ya uchekeshaji na kilikuwa kianze kuruka katika moja ya Televisheni, lakini kutokana na hali aliyo nayo hawezi kuigiza.

Hali yangu hii inanifanya nishindwe kabisa kuendelea na ajira yangu ya uigizaji," alisema.

"Kwangu ni tofauti na wenzangu ambao husimama kuigiza baada ya kukataliwa na waume zao, lakini mimi nasimama kutokana na hali yangu.

"Pia nahitaji kumlea mtoto wangu ajaye, nahitaji kupumzika zaidi. Ninasimama kuigiza hadi hapo mwanangu atakapokua.
Msanii huyo ameigiza filamu mbalimbali zikiwamo The Hero Of Church ya Steven Kanumba. Nyingine ni Umenicheki, Piga Ua, Gentleman pamoja na Orange Girl.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms