Monday, June 18, 2012

......SIWEZI KUFIKIA KIWANGO CHA MARIA CAREY.....

MWIMBAJI Cheryl Cole, amesema anafahamu kwamba hawezi kuimba vizuri kufikia kiwango cha Mariah Carey, lakini hivi majuzi aliimba live na kuwashangaa wale wanaosema huwa anaimba kwa kufuatisha cd.

Cheryl aliandamwa na mashabiki wake waliopo katika mtandao wa twitter wakisema kuwa aliimba kwa kutumia cd huku akidanganya kwa kuwa na wapiga vyombo nyuma yake.

"Ninajua uwezo wangu wa kuimba hauwezi kufikia wa Mariah Carey, lakini si kweli kuwa sikuimba live, ila ninashukuru kwa kuwa hii inaonyesha ni kiasi gani sauti yangu ni nzuri na uwezo wa kuimba umeongezeka," alisema Cheryl.

Aliongeza kusema mashabiki wake watarajie maajabu zaidi katika albamu yake ya pili, akisema kuwa ni bora kwani sasa amekua kiakili, kiumri na kisanii.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms