Friday, June 1, 2012

.....SIJAPEWA TALAKA JAMANI, BADO NI MKE HALALI.....


IYABO Ojo amekiri kuwa bado hajapata talaka yake na kisheria anatambulika kuwa mke halali wa Deroju Ojo, ingawa hawaishi pamoja tena.

"Lakini hiyo hainizuii kuishi maisha yangu, sina haraka ya kuolewa tena. Hata kama nikipata talaka yangu leo sidhani kama nitafanya maamuzi mapya haraka,"alisema.

"Siwezi kuliacha jina la Ojo kwa haraka kwa vile imekuwa kama utambulisho wangu na limefahamika sana, nitatumia hilo jina pia kwa heshima ya watoto wangu."

Lakini alipoulizwa kama hatakuwa akikiuka kwa kutumia jina la mtu ambaye wameachana, alisema:

"Kila mtu anaweza kuwa Ojo, kuna familia nyingi sana kwenye huo ukoo na wataniheshimu kwa vile nimeendelea kulithamini jina lao, usisahau kwamba nina damu yao tayari."

Msanii huyo iliripotiwa kufarakana na mumewe kwa vile kila mmoja alikuwa akimtuhumu mwenzake kwa kuwa na uhusiano wa nje.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms