Tuesday, June 12, 2012

.....SHERYL CROWN APATA KANSA NYINGINE....


MWIMBAJI, Sheryl Crow, ametangaza kuwa ana kansa ya ubongo, lakini amewataka mashabiki wake wasiwe na wasiwasi kwani ipo katika hatua za awali.

Crow ambaye nyimbo zake maarufu ni pamoja na All I Wanna Do na Soak Up The Sun, aligundulika kuwa na kansa hiyo mwishoni mwa mwaka jana baada ya kufanikiwa kuitibu kansa ya matiti miaka kadhaa iliyopita.

Anasema alifanyiwa vipimo baada ya kuwa anasumbuliwa na tatizo la kupoteza kumbukumbu mara kwa mara.

Anaongeza kuwa ilifikia wakati alisahau mashairi ya wimbo wakati akifanya shoo huko Las Vegas, ilikuwa mwanzoni mwa mwaka jana.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms