Monday, June 11, 2012

.......PRINCESS GETRUDE ATOA MESEJI NZITO KWA WASANII WENZAKE........


 PICHA JUU NA NI PRINCESS GETRUDE

Msanii chipikizi nchini (ambaye pia ni hot model wa blog hii)  anayejulikana kwa jina la Princess Getrude amefunguka na kusema kwamba, wasanii ni muhimu sana katika ukuaji wa tasnia ya filamu nchini na kwahiyo kuwaomba wasanii wote kutokwenda kinyume na destruti yetu ya Kitanzania. Akichonga na blog hii msanii huyu ambaye kwa muda wote alioneka kuwa mpole na mwenye hekima, alisema kuwa kazi ya sanaa ni kazi kama kazi nyingine.
"Sisi wasanii ni kama wafanya kazi wengine, kwahiyo tunahitaji kuheshimiwa pia" aliongeza msanii huyo. hata hivyo aliongeza kuwa pamoja na heshima ambayo tunastahili kuipata kutoka kwenye jamii lakini pia na sisi kama wasanii tunatakiwa kujiheshimu na kufanya matendo mema mbele ya watanzania wengine na yanayokubaliwa na Watanzania.....
Msanii huyu ambaye muda si mrefu utaanza kumuona kwenye luninga kwenye tamthiliya moja ambayo hakuwa tayari kuitaja kwa sasa. Aliongeza kuwa pia yuko mbioni kuandaa filamu yake ambayo anaamini kwa itakimbiza sana mtaani.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms