Thursday, June 14, 2012

.......NINAYE WANGU JAMANI SITAKI USUMBUFU....


MWIGIZAJI wa filamu anayeibukia Swahiliwood Halima Ali, amesisitiza kuwa anaye wake tofauti na watu wanavyofikiria, hivyo hataki kusumbuliwa.

Anasema kweli wengi wanajua ni binti mdogo ambaye pengine anahitaji kuwa na mahusiano na mtu mwingine.
Lakini anasema hahitaji mpenzi kwani tayari ana mchumba na hayupo huru kwa ajili ya mtu mwingine.

Anasema usumbufu ameanza kuupata baada ya filamu ya Lap Top kutoka, ndipo wanaume kadhaa wameanza kumsumbua kwa kutaka kuanzisha uhusiano naye.

"Mara nyingi sisi wasanii hasa wa kike tunakabiliwa na vishawishi vingi, yaani watu hudhani ni watu huru tusiona na uhusiano. Jamani kwangu haipo hivyo, nina mchumba," alisema.

"Unajua tangu ilipotoka filamu ya Lap Top nimepata marafiki wengi, lakini wanaume wananitaka kimapenzi.
"Jamani nawaambia tayari nina mchumba ambaye ninampenda sana."

Katika Lap Top, msanii huyo anaonekana akiwa mwanafunzi anayenyanyaswa kimapenzi na kiasi cha kutembea wanaume wengi ili wasisambaze picha zake za utupu.

Mbali ya Lap Top inayofanya vizuri sokoni, Halima pia ameshiriki katika filamu za The Diplomat, Hard Time, Royal Family na Tell The Truth.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms