Wednesday, June 6, 2012

......MAJUNGU HAYAJENGI.....


MTAYARISHAJI na Muongozaji wa filamu Swahiliwood Vincent Kigosi 'Ray' amewaambia wasanii wa Bongo, kufanya kazi na kuachana na tabia za majungu.

Binafsi sipendi sana kuongelea mambo ya mtu zaidi ya kazi yangu ninayoifanya ya filamu na si maisha ya watu binafsi kwani inawezekana kila mtu ana upungufu wake kama binadamu, msanii mwenzako akikosea jaribu kumweleza kabla ya kwenda kuongea na vyombo vya habari,alisema Ray.

Ray alisema kuna baadhi ya wasanii wanatumia vyombo vya habari vibaya kwa kutoa taarifa zinazochafua tasnia hiyo huku wakisahau kuwa kwa kufanya hivyo tatizo hivyo wote wanachafuka na jamii inaweza kuwadharau na kuharibu hata soko la filamu.

Ray alisisitiza kuwa likitokea jambo wazungumze na kushauriana kabla ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms