Thursday, June 14, 2012

.........MABADILIKO KATIKA TASNIA YA FILAMU YANAHITAJIKA SANA.......


MTAYARISHAJI wa filamu za Swahiliwood, Chrissent Mhenga Uncle Chriss, amesema kuwa tasnia ya filamu inahitaji mabadiliko makubwa ili ilete tija na maslahi kwa watayarishaji na wasanii husika.
Ukweli haupingiki kuwa wasanii wote hapa Tanzania wametoka katika kundi la Kaole ambalo mimi nilikuwa Mkurugenzi wake," anasema.
"Niliweza kuwajenga na wameweza kuliteka soko la tasnia ya filamu hivi sasa, lakini kuna jambo moja tu ambalo naliona ni tatizo. Hadithi hazishiki watu kwa muda mrefu tofauti na awali nilipokuwa nikiandikia wasanii hawa katika kundi la Kaole."
Hivyo amewasisitizia wasanii kujitahidi kujifunza vitu vya kitaaluma akisema filamu nyingi za siku hizi zimekuwa zikikosa uhalisi kwa kukosa taarifa kwa wahusika kuhusiana na jambo linachezwa katika filamu.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms