Thursday, June 28, 2012

.......KUNA MTU ANANIZUSHIA NA KUNICHOKONOA.......


MWIGIZAJI nyota katika tasnia ya filamu za Swahiliwood, Jacqueline Wolper, amedai kuna mtangazaji mmoja wa Bongo anayemchafua makusudi kwa kumzushia kashfa mbalimbali.

Alisema kuwa mtangazaji huyo wa kike, pia anajaribu kumtengenezea mazingira ya yeye kuingia katika ugomvi na wasanii wenzake wa kike.

Jack amesema hayo baada ya kuenea kwa uvumi kuwa amenyang'anywa gari aina BMX 6 aliyopewa na mpenzi wake na amezuiwa kukata mitaa.

Anaeneza habari za uzushi ikiwa na kuhakikisha kuwa mimi ninakosa na wasanii wenzangu, kama hivi karibuni nikiwa kwenye sehemu za kupigia picha na rafiki zangu walinipigia simu wakinijulisha kuna habari zinatangazwa eti nimenyang'anywa gari," alisema.

"Hizi ni habari za uongo mtupu. Si kweli, kwani gari lipo ndani nyumbani kwangu."

Msanii huyo amedai kuwa anamiliki gari zaidi ya moja kwa hiyo hakuna mtu wa kumpangia atembelee gari gani, kwani katika taarifa hizo ilisemekana kuwa kuwa alikuwa akitembelea gari aina ya Noah.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms