Thursday, June 28, 2012

........KATIKA PICHA JINSI HALI ILIVYOKUWA BAADA YA DKT ULIMBOKA KUFIKISHWA MUHIMBILI........

Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakiisukuma gari iliyokuwa imempaki Dk. Stevan Ulimboka.
Madaktari na Wauguzi wa Muhimbili wakiwa wamesimama huku wakizungumzia hali iliyompaka mwenzao.

Hakuna kazi iliyokuwa ikifanyika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati Dk. Ulimboka akifikishwa hospitalini hapo.


Wanahabari wakitafuta taswira.


Picha zote na matukio michuzi blog


...KAMA KOVA AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI...

Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova amezungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo la utekaji nyara na kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.
Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezi kuwa msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.
Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutoke nchini, ameongeza kwamba wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo wachukuliwa hatua za kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms