Tuesday, June 19, 2012

......HADITHI ZA DINI NA CLOUD NI DAMU DAMU....


MWONGOZAJI, mwigizaji na mtayarishaji wa filamu Swahiliwood, Issa Mussa Cloud 112, anasema kuandaa filamu inayohusu hadithi za dini ni kazi ngumu, lakini ndiyo inayombeba.

Amesema katika filamu zote alizowahi kuigiza, hajawahi kupongezwa kama anavyopongezwa katika filamu yake mpya ya Toba inayozungumzia mambo ya kidini.

Kwa sasa nina mtihani mkubwa, baada ya kutoka filamu ya Toba iliyowagusa wengi, watu wanataka niendelee nazo, lakini shida inayonikabili ugumu wa filamu za aina hii," alisema.

"Ni filamu zinazohitaji fedha nyingi katika kurekodi, fedha hizo ni kwa ajili ya mavazi na malipo kwa wahusika si jambo dogo.

Filamu ya Toba ilizinduliwa hivi karibuni katika ukumbi wa Ngome Kongwe mjini Unguja, Zanzibar na kuhudhuriwa na Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad na viongozi wengine kadhaa.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms