Friday, June 29, 2012

........FILAMU YA KOMAMNDO YOSSO SIIPENDI......


BIGGIE amekiri kuwa katika filamu alizocheza, kuna ile ya Komando Yosso akisema haipendi na hataki hata kuiona.
Katika maisha kila msanii au binadamu yeyote anapenda kusifiwa kwa kazi aliyoifanya, lakini katika kazi zangu zote nilizowahi kushiriki, filamu mbaya kwangu ni ile ya Komando Yosso," alisema.

"Baada ya kuicheza nilifanikiwa kuangalia sehemu kidogo tu katika CD ya pili, sikutaka kuiangalia tena, ni filamu ambayo nilisema najuta kushiriki japo nilikuwa najua hadithi yake lakini matokeo hayakuwa vile."

Biggie amesema kuwa mara nyingi watayarishaji hawataki ushauri kutoka kwa msanii wakiamini kuwa wao ndio kila kitu, kwa sasa ameamua kuwa kabla ya kuingia na kushiriki filamu yoyote lazima asome muswada wote na kuwatambua watendaji kama mpiga picha hata Mwongozaji.

Anasema hivyo kwa vile anaamini kuwa wao wana mchango mkubwa katika utengenezaji wa filamu.

Msanii huyo kwa sasa anaigiza filamu ya Injinia ya Kipemba baada ya kuridhika na muswada wa filamu hiyo.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms