Tuesday, June 26, 2012

......BABA NA MWANA MALUMBANO KAMA KAWA.....


MALUMBANO kati ya mwimbaji, Christina Aguilera na baba yake Fausto, si jambo jipya katika vyombo vya habari.

Kila mmoja anamlaumu mwenzake kwa kuwa kikwazo katika kutafuta suluhu.

Wakati hilo likiwa halijapatiwa ufumbuzi, ndugu wengine wa karibu wameamua kumtafuta mwanamuziki huyo ili awape msaada bibi na babu yake wanaoelezewa kuwa wagonjwa sana.

Baba mdogo wa mwanamuziki huyu, Johann Aguilera, amesema bibi na babu wa staa huyo wanasisitiza kuwa wanataka kumwona mjukuu wao kabla hawajaaga dunia.

"Babu yake ana umri wa miaka 86 na bibi ana miaka 82, wote kilio chao ni kutaka kumwona mjukuu wao na mtoto wake Max kabla hawajafa," alisema Johann.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Design by Free WordPress Themes | Bloggerized by Lasantha - Premium Blogger Themes | Grants For Single Moms